18 Aprili 2020 - 10:37
Rais Rouhani atuma ujumbe kwa mnasaba wa Siku ya Jeshi: Jeshi ni mlinzi wa roho za Wairani

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma ujumbe kwa mnasaba wa Siku ya Jeshi ambayo inaadhimishwa leo tarehe 29 mwezi Farvardin na kusisitiza kuwa, jeshi la taifa ni mlinzi wa roho za Wairani katika vita na amani, katika vita laini na ngumu, katika medani ya vita, mitaani, makambini na mahospitalini.

(ABNA24.com) Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hayo katika ujumbe wake uliosomwa na Brigedia Jenerali Amir Hatami Waziri wa Ulinzi wa Iran mbele ya gwaride la jeshi kuongeza kuwa: Ingawa katika siku hizi za kulinda roho za binadamu nchini Iran na katika maeneo yote ya dunia haiwezekani kufanyika gwaride la vikosi vya jeshi kwa mujibu wa protokali za kiafya na kijamii, lakini raia wa Iran wakiwa nyumbani na wanaharakati wote wa kicuhumi na kijamii katika sehemu zao za kazi wanashuhudia kwa macho maneva ya uwezo wa kitaifa na kijamii wa walinzi wa nchi na wasaidizi wa afya na wanalipongeza na kulitakia kheri jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wahudumu wa sekta ya afya.   

Katika ujumbe wake huo, Rais Rouhani amesema, harakati inayoungwa mkono na wananchi, jeshi na vikosi vya ulinzi ni lazima iibuke na ushindi.

Ujumbe huo wa  Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aidha umeongeza kuwa: Suala la kujilinda na kukabiliana na adui siku zote ni moja ya mazuri ya maisha ya wanadamu katika zama za uhai wa kiumbe huyo na leo hii uzuri huo pia unashuhudiwa vyema katika kukabiliana na adui wa wazi na aliyejificha.  

Rais Rouhani ameongeza kuwa jeshi la Iran si tu ni nembo ya vita vya wananchi bali ni dhihirisho la uungaji mkono wa taifa na maslahi ya taifa.   

Amesema hii leo makamanda na wakuu wa jeshi la Iran wanatengeneza hamasa kwa kushirikiana na walinzi na wahudumu wa afya wanaolinda maisha ya wananchi.

Maadhimisho ya Siku ya Jeshi hapa nchini yamefanyika mapema leo hapa Tehran na katika makao makuu ya mikoa 24 yakihudhuriwa na makamanda wa vikosi vya jeshi. Maadhimisho hayo yamefanyika chini ya  kauli mbiu ya "Walinzi wa Nchi- Wasaidizi wa Afya."  

Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kila mwaka tarehe 29 Farvardin kwa kalenda ya mwaka wa Kiirani ambayo ni sawa na 17 Aprili huandaa gwaride katika maeneo yote ya Iran ya Kiislamu ambapo huonyesha mafanikio yake ya kiulinzi na kijeshi kwa mnasaba wa 'Siku ya Jeshi'.

............
340